Bunge la Zambia limemsimamisha waziri
kwa muda wa mwezi mmoja asihudhurie vikao kutokana na kosa la kumpiga
mbunge kwenye viwanja vya Bunge.
Spika wa Bunge la Taifa, Patrick
Matibini amesema Waziri wa Jimbo la Lusaka, Bowman Lusambo amesimamishwa
baada ya kumchapa kibao mbunge Chishimba Kambwili hapo Oktoba mwaka
jana, na kusema kwamba tabia hiyo haikubaliki dhidi ya mbunge.
"Hili ni Bunge la heshima, nina wajibu
wa kuhakikisha kwamba heshima na haiba ya Bunge inalindwa na
inahifadhiwa wakati wote," amesema spika huyo.
Kutokana na kusimamishwa huko Waziri Lusambo hatapata marupurupu na mshahara kama mbunge kwa mwezi wote anaotumikia adhabu.
Imeelezwa kwamba ni jambo la kawaida kwa
wabunge kutumia lugha isiyofaa na kuleta mizozo, lakini kwa kitendo cha
Waziri kumpiga mbunge hakikuwa cha kuvumilika.
No comments:
Post a Comment