WALIMU
wakuu wa skuli za Zanzibar wametakiwa kutambua hadhi ya elimu ya
maandalizi badala ya kuipa kisogo na kuwatenga walimu wanaosomesha
madarasa hayo.
Ofisa
Mdhamini wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Elimu Pemba Salum Kitwana
Sururu, amesema elimu hiyo ndio msingi mzuri wa kumjenga mtoto.
Akizungumza
na washiriki wa kikao cha tathmini ya mradi wa ‘Watoto Kwanza’
uliolenga kuwaandaa walimu wa skuli za maandalizi unaohitimisha miaka
minne kilichofanyika hoteli ya Mazson, Sururu alisema Serikali ya
Mapinduzi Zanzibar mwaka 2006 ilitangaza sera ya ulazima wa elimu ya
maandalizi kwa watoto kuanzia miaka minne hadi mitano.
Alifahamisha
kuwa, ufahamu mzuri wa wanafunzi wa msingi na sekondari, hutokana na
kupitia madarasa ya maandalizi ambako hufinyangwa na kuandaliwa njia
njema ya kupata ufanisi katika masomo yao.
Sururu
alisema si sifa njema pale walimu wakuu wanaotegemewa kuwa
washaajishaji wa sera ya elimu ya maandalizi, wawe mstari wa mbele
kuwapuuza walimu waliofundishwa kwa ajili ya madarasa hayo.
Alieleza
masikitiko yake kwamba bado kuna kundi ambalo haliko tayari kuipa elimu
ya maandalizi wala walimu wa madarasa hayo haki wanayostahiki kwa
manufaa ya watoto ambao kimsingi ndio walimu, wataalamu na viongozi wa
kesho.
Aidha
ofisa huyo aliwataka walimu kubadilika na kushirikiana kwa pamoja ili
kuhakikisha sera ya elimu ya maandalizi inapata mafanikio kama
ilivyokusudiwa na serikali.
“Tufike
pahala tujue thamani ya fedha zinazotolewa na wafadhili kwa mamilioni
kwa ajili ya kuisaidia nchi yetu kuendeleza sekta ya elimu, tuoneshe
utayari wetu katika kuleta matokeo chanya,” alisisitiza.
No comments:
Post a Comment