MLINZI wa Hospitali ya Kanisa Katoliki la Kijiji cha Mwanzugi wilayani Igunga, Peter Marco apata kifungo cha miaka 30 gerezani kwa kosa la kumuibia kwa kutumia silaha Sista Aline Nicette vitu kadhaa, ikiwamo simu ya mkononi, vyote vikiwa na thamani ya Tsh.720,000/-
Mahakimu Augustine Mwarija, Lugano Mwandambo na Lilian Mashaka walitupilia rufaa ambayo Marco, mrufani, aliwasilisha kupinga hukumu iliyotolewa na Mahakama Kuu.
“Tumeridhika kwamba ushahidi ulithibitisha kesi dhidi ya Marco bila shaka yoyote, kiwango cha uthibitisho kinachotumika katika kesi za jinai. Hatuoni umuhimu wa kukata rufaa na tumeitupilia mbali,” walisema katika hukumu yao waliyoitoa Tabora hivi karibuni.
Wakati wa kusikilizwa kwa rufaa hiyo, Marco alilalamika kuwa ushahidi wa utambulisho wa vielelezo kupitia mashahidi wawili wa upande wa mashtaka ambao ni Mlinzi na Sista Aline uliotegemewa na Mahakama Kuu kuthibitisha hukumu yake ya unyang’anyi wa kutumia silaha unatia shaka na kesi inayomkabili haikuthibitishwa.
Shahidi wa tukio hilo ambae alikuwa mlinzi mwenza wa mtuhumiwa(Marco) alisema majambazi nane walivamia kanisani hapo, huku wanne wakiwa na mapanga. Alifanikiwa kumtambua Marco ambaye alimuona akiwa ameshika panga na bunduki.
No comments:
Post a Comment