Maharamia wa kazi za wasanii zaidi ya 200 waliokamatwa katika zoezi laukamataji kazi feki za sanaa wanatarajiwa kufikishwa mahakamani wiki ijayo.
Akizungumza jijini Dar es
Salaam, Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Auction Mart, Alex Msama amesema
kuwa kwa sasa anaishukuru serikali kwa ushirikiano ambao wamekuwa
wakiuonyesha kwa kuwa bega kwa bega kwa vile wamekuwa wakinyonya
wasanii.
“Ndugu zangu waandishi nimewaita
hapa kuwaeleza juu ya zoezi la kumkamata maharamia wa kazi za sanaa
bado linaendelea vizuri na sasa wanatarajia kufikishwa mahakamani wiki
ijayo ili waweze kusomewa mashtaka yao,” Alisema Msama.
Msama alisema kuwa mpaka sasa
msako huo umefanikisha kukamata vifaa vya zaidi ya bilioni 1 ambavyo
ikiwemo kopyuta, laptop na cd feki.
Aliongeza kuwa watanzania lazima
walipe kodi na wauze kazi zilizo na stika za mapato (TRA) ili wasanii
wapate mapato na serikali ipate mapato.
“Wamachinga acheni kulalamika,
mnaopoenda kununua Filamu za nje na ndani hakikisheni Filamu hiyo ina
Stika ya TRA, ukiuza yenye Stika mtu hatokukamata”, amesema Msama.
Msama aliwaomba Watanzania
watambue awamu hii ya Tano ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli haitaki
ujanja ujanja, lazima kufanya kazi kwa bidii ili upate kipato halali.
Hata hivyo, zoezi laukamataji Kazi feki za sanaa litaendelea katika Mkoa wa Morogoro, ikiwa ni zoezi la nchi nzima.
No comments:
Post a Comment