Naibu Waziri wa OR TAMISEMI Mh.
Josephat Sinkamba Kandege ametoa maagizo 14 kwa Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa
Wilaya na Wakurugenzi wote Tanzania bara ili kuboresha upatikanaji bora
wa huduma za kijamii katika maeneo yao na kuondoa changamoto zilizopo.
Ametoa
maagizo hayo katika majumuisho ya ziara yake ya siku 10 katika mkoa wa
Rukwa yaliyowakutanisha watumishi wa Halmashauri Nne za Mkoa wa Rukwa
yaliyofanyika katika Ukumbi wa Manispaa ya Sumbawanga ambapo ni makao
makuu ya Mkoa huo.
Maagizo
hayo yamekuja baada ya Kutembelea miradi kadhaa katika Wilaya tatu za
Mkoa na kubaini mambo ambayo yanakwamisha maendeleo ya wananchi wa mkoa
huo na taifa kwa jumla.
Yafuatayo maagizo yake.
1.
Watumishi wa umma kufanya kazi kwa bidi kujituma kwa weledi mkubwa ili
kuwa na utumishi wenye matokeo kukosekana kwa huduma hiyo iliyobora
kunafifisha jitihada za wananchi katika kutafuta na kujiletea maendeleo
hivyo ni vyema watumishi wa umma wakajitathmini wao binafsi kuona endapo
wanaridhika na huduma wanayoitoa kwa jamii na kuchukua hatua ya
kubadilika.
2.
Wakurugenzi wa Halmashauri wahakikishe kuwa wanashughulikia haki
stahili za watumishi kwa wakati na kwa kuzingatia sheria kanuni na
taratibu, ipo tabia ambayo imeanza kujengeka kwa waajiri kutolipa
stahili kwa visingizia kwamba madai hayo yamewekwa kwenhye orodha ya
madeni, tabia hii haikubaliki katika uongozi wa sasa. Maelekezo ya
serikali ni kwamba waajiri wote wahakikishe hawazalishi madeni badala
yake watenge fedha za kustosha kulipia gharama hizo. Makatibu tawala wa
mikoa wahakikishe wanahakiki madeni yote yanayopokelewa kutoka
halmashauri kabla ya kuwasilisha serikali kuu.
3.
Wakurugenzi wote wa Halmashauri wahakikishe wanajaza nafasi zilizowazi
za wakuu wa idara na vitengo kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu
zilizopo, baadhi ya Halmashauri watumishi wanakaimu nafasi hizo kwa muda
mrefu. Hivyo hudumaza utoaji huduma wa idara. Makatibu tawala wa mikoa
wasiamamie jambo hili na endapo kutakosekana maafisa wenye sifa
wayawasilishe maomb I hayo ya maafisa wenye sifa kwenye OR TAMISEMI.
4.
Wakuu wa Mikoa yote Tanzania bara kuhakikisha na kusimamia Halmashauri
zote ambazo zina hoja za ukaguzi na maagizo ya kamati za bunge na
serikali za mitaa (LAAC) zinajibiwa na kuwasilisha majibu ya hoja hizo
na kuyawasilisha Ofisi ya CAG kwa mjuda uliopangwa, Halmashauri ya
Wilaya ya Nkasi na Manispaa ya Sumbawanga ni miongoni mwa Halmashauri
Mahususi zilizopewa maagizo na Kamati ya LAAC.
5.
Mkoa wa Rukwa uhakikishe kwamba kuanzia mwaka wa masomo 2018 unaanzisha
na kuendeleza mpango wa wanafunzi kula chakula wakiwa shuleni kutokana
na ziada ya uzalishaji wa chakula iliyopatikana
6.
Wataalamu wa Sekta ya ardhi wahakikishe wanatatua kero na migogoro ya
Ardhi kwa kuandaa mipango ya matumizi bora ya ardhi za vijiji na mipango
miji, aidha wanatakiwa kuwa mbele ya wakati kwa kutambua na kupanga
miji hasa inayoibuka ambayo iko chini ya sheria za ardhi ili kuzuia
ujenzi holela na kuwa na miji isiyopangika, samabamba na hili
wahakikishe wanashirikiana na idara za ujenzi na afya ili kuhakikisha
kuwa nyumba zote zinazojengwa mijini zimepata kibali cha ujenzi,
halmashauri zihakikishe zinatenga fedha za kutosha kwa mwaka wa fedha
2018/2019 kutekeleza jambo hili.
7.
Halmashauri zote zihakikishe kwamba majengo yote ya taasisi za umma
hasa vituo vya kutolea huduma za afya na shule yanapimwa na kupatiwa
hati ili kuepusha migogoro na jamii inayozunguka maeneo hayo.
8.
Mameneja wote wa TARURA Tanzania bara wafanye kazi kwa kushirikiana na
Halmashauri, mipango ya ujenzi na matengenezo ya barabara itokane na
maamuzi na vipaumbele vya Halmashauri isipokuwa Wakala waweke kipaumbele
kulingana na bajeti iliyopo. Aidha Dhana ambayo imeanza kujengeka kwa
baadhi ya watendaji wa TARURA kuwa wakala ni chombo huru hivyo
hakiingiliwi ni dhana potofu.
9.
Halmashauri zihakikishe kwamba zinatumia Force Account kwa miradi yote
ya ujenzi ambayo utaalamu na ujuzi wake vinapatikana katika mazingira ya
miradi husika inapotekeleza ili kuharakisha utekelezaji wa miradi hii
ili kuounguza gharama pamoja na kutoa ajira kwa jamii inayozunguka
miradi hiyo.
10.
Kutokana na upungufu mkubwa wa watumishi ulioripotiwa na Halmashauri
katika vituo vya kutolea huduma, Shule, huduma za afya na ofisi za
watendaji wa kata na vijiji kutokana na sababu mbalimbali kama zoezi la
uhakiki na baadhi kuhamia TARURA, Mikoa ifanye tathmini ya awali ya
mgawanyo wa watumishi ndani ya mikoa na halmashauri kubaini maeneo yenye
ziada na upungufu kufanya mgawango sawia wa watumishi kabla ya
kuwasilisha maombi hayo kwa OR – TAMISEMI, maombi hayo yaambatane na
maombi ya watumishi wa kada hiyo ndani ya Mkoa.
11.
Kutokana na muitikio wa uchangiaji mdgogo wa wananchi katika mfuko wa
afya ya jamii (CHF) Halmashauri zinaelekezwa kuendelea kuhamasisha jamii
umuhimu wa kuchangia mfuko. Mganga Mkuu wa Mkoa na Halmashauri
wanaagizwa kuwa hadi kufikia Mwisho wa Mwaka wa Fedha 2017/2018
uchangiaji wa CHF uwe umefikia Walau asilimia 50
12.
Wakurugenzi wote Tanzania Bara wahakikishe wanatambua na kujaza nafasi
zote zilizowazi za uongozi katika serikali za vijiji na mitaa hadi
kufikia Juni 2018. Aidha Mikoa iandae na kuwasilisha OR TAMISEMI Orodha
ya nafasi wazi za viongozi katika ngazi hizi.
13.
Wakurugenzi wa Halmashauri Tanzania Bara kupitia wakaguzi wa ndani wa
halmashauri wahakikishe kuwa wanafanya ukaguzi wa hesabu za kata,
vijiji, vituo vya kutolea huduma ikiwemo vituo vya afya, zahanati na
shule katika kila robo na kujadili katika vikao halali vya halmashauri
kwakuwa takwa hili ni la kisheria chini ya sheria ya fedha ya Mamlaka ya
Serikali za Mitaa Sura 290 kuliko suala hili sasa hivi limeachwa kwenye
mikutano mikuu ya vijiji ambavyo haifanyiki ipasavyo. Kamati za vituo
vya kutolea huduma haziwasilishi taarifa hizo kwenye kata na vijiji.
14.
Mkoa wa Rukwa uhakikishe kuwa tunaendelea kutunza, kuhifadhi na
kuendeleza ng’ombe wenye asili ya kifipa, ng’ombe hawa wana uwezo wa
kustahimili magonjwa na uwezo mkubwa wa kushiriki kwenye nguvu kazi kwa
maana ya shughuli za kilimo. Mikoa mingine lazima kufunga zaidi ya jozi
“pear” moja lakini kwa huku jozi moja inatosha hivyo ni vizuri
tukahakikisha kwamba ng’ombe hawa wenye asili ya kifipa tunwalinda
kuwahifadhi na kuwaendeleza.
No comments:
Post a Comment